HIZI NDIYO SABABU ZA HUMUD KUONDOKA MAJIMAJI FC
Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru |
WIKI kadhaa baada ya kiungo mkabaji Abdulhalim Humud kutangaza
kujiondoa kwenye kikosi cha Majimaji, hatimaye klabu hiyo imetoa jibu
kuhusu Humud.
Humud, kiungo wa zamani wa Simba na Coastal Union alisajiliwa na
Majimaji mwanzoni mwa msimu huu wa 2017/18 lakini hakudumu muda mrefu
na ikaelezwa kuwa ameondoka kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri
na uongozi wa Majimaji.
Akizungumzia juu ya hali hiyo, Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo
Ndunguru, alisema ni kweli Humud hayupo lakini yeye mchezaji ndiye
ambaye aliyeomba kuachwa kutokana na sababu za kifamilia.
“Humud ni kweli hatutakuwa naye, hiyo ni rasmi, yeye ndiye
aliyeandika barua ya kuomba kuondoka Majimaji, alisema ana matatizo
ya kifamilia na hataweza kuwa mbali na familia yake.
“TFF wameshaandika barua kwa Majimaji na Majimaji imeshajibu kwa
kutoa barua ya kumuacha na kilichokuwa kimebakia ni kupatiwa haki
zake,” alisema Ofisa Habari huyo.
Post a Comment