ad

ad

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 26 KUGAWIWA WANAHISA WA VODACOM


Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC wakifuatilia
mada wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa hao
uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.

Mmoja wa wanahisa za Vodacom Tanzania PLC ,akichangia mada
wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa hao uliofanyika
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wanahisa za Vodacom Tanzania PLC,wakibadilishana
mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian
Ferrao (kulia)wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa hao
uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.

Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki (kulia)
akisalimiana na mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo, Adella Kaale,wakati
wa Mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa hao uliofanyika katika uwanja
wa taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao
(kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari( hawapo
pichani) juu ya Mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa kampuni
hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki, Katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Ali
Mafuruki na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo,Jacgues Marais.

Zaidi ya wanahisa 1500 wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC,Walikutana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki na kufanya mkutano  na Uongozi wa kampuni hiyo na  kuchagua viongozi mbalimbali na kufikia mwaafaka wa gawio la kwanza la Hisa kwa wanachama hao utakaotolewa na kampuni hiyo  kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 26 ifikapo mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.


Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,na Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki alipokuwa akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa gawio hilo kwa wanahisa wake.


Mwenyekiti huyo wa bodi alisema kwamba kila mwana hisa atapatiwa gawio hilo la shilingi 12 na senti 74.



Aidha alisema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo kutokana na kuimarika vizuri kwa kujiendesha kibiashara hivyo iliona ni vyema kutoa gawio hilo, ili kila mwanahisa aweze kunufaika pale inapobidi.


Kampuni hiyo pia iliweza kufanya mkutano wake Mkuu wa mwaka kwa kuwakutanisha wanachama wake kutoka mikoa mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kwenda sambamba na uteuzi wa wajumbe wapya watakaoingia ndani ya bodi ya wakurugenzi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Ian Ferrao  aliwapongeza wajumbe wote walioteuliwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha hisa za vodacom zinaleta manufaa kwa wamiliki wake wote.


“Wanahisa watoe shaka kabisa kuhusiana na hisa zao kwani zipo salama na kampuni inaendelea kufanya vizuri sokoni na ninawapongeza wajumbe walioteuliwa na ninaimani nayo  kwani itafanya kazi kwa kushirikiana vizuri  na wanachama ndani nasi tutawapa ushirikiano wakutosha ndani ya kampuni yetu”Alisema Ferrao.

No comments

Powered by Blogger.