Balozi
wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe, Sylvester
Mabumba (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji wa Comoro, Bw. Said Mohamed Omar
(wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds
Media Group pamoja na wajumbe waliofuatana nao katika ziara maalum ya
kufungua na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania na Comoro.
Balozi
wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya comoro pamoja na Wajumbe
kutoka clouds Media Group wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Comoro, Bw. Mouzamildine Youssouf.
BALOZI
wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Sylvester Mabumba
ameupokea ujumbe wa Clouds Media Group uliowasili visiwani humo Januari
20 mwaka 2018.
Upo
kwenye ziara maalumu ya siku tatu ikiwa na lengo la kushirikiana na
ubalozi kuzitangaza fursa mbalimbali zinazopatikana visiwani humo kwa
Watanzania. Ujumbe
huo wa Clouds Media Group ukiongozwa na Mkurugenzi wa vipindi na
uzalishaji, Ruge Mutahaba uliwasili Comoro kutokana na mualiko wa
Ubalozi wa Tanzania hapa Comoro
Ambapo
lengo lake lilikuwa ni kuja kufanya tathamini ya kuzindua Jukwa la
Fursa (FURSA EXPO) Visiwani Comoro kama sehemu ya kuendeleza kampeni za
kuwapatia vijana wa kitanzania taarifa muhimu kuhusu fursa za uwekezaji
na biashara.
Ubalozi
wa Tanzania Visiwani Comoro kwa kushirikiana na Ujumbe wa Clouds Media
Group umelenga ifikapo Aprili mwaka 2018 kupanua mianya ya uwekezaji
nchini Comoro na kuhakikisha masoko ya uhakika yanapatikana kwa ajili ya
bidhaa za Tanzania hasa katika kipindi hiki ambapo Uchumi wa Tanzania
unaelekea kuwa ni uchumi wa Viwanda.
Aidha,
Balozi akiwa ameambatana na ujumbe wa Clouds Media Group amepata fursa
ya kuonana na kufanya mazungumzo na wadau kutoka sekta mbalimbali za
Serikali ya Comoro, Mashirika ya Umma na Sekta Binafsi. “Serikali
ya Tanzania itaendelea kufungua maeneo mapya ya ushirikiano sambamba na
kuhakikisha vijana wananufaika na ushirikiano baina ya nchi na nchi
ulioanzishwa na mataifa yao” mesema Balozi
Aidha,
Mhe. Balozi alielezea anataraji ziara hiyo italeta matokeo chanya na
kwamba kuzinduliwa kwa jukwaa la FURSA EXPO ni sehemu mojawapo ya
utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ambayo inalenga kwenye Diplomasia ya
Uchumi na kwamba kupitia jukwaa hilo bidhaa za Tanzania zinauhakika wa
kuingia kwenye Soko la Comoro kwani nchi ya Comoro inaitegemea Tanzania
kwa kiasi kikubwa katika mahitaji yake mbalimbali.
Pia
ujumbe wa Clouds Media Group ulitumia nafasi hiyo kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Visiwani Comoro, Ndg. Said
Mohamed Omar, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Kitaifa ya Utalii, Ndg.
Mouzamildine Youssouf pamoja na Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Vijana.
Katika mazungumzo hayo, wajumbe walionesha nia ya kutaka kushirikiana
kwa pamoja katika kuendesha kampeni itakayoibua maeneo muhimu ya
kimkakati ambayo Vijana wa Kitanzania na wale wa KiComoro wanaweza
kushirikiana.
Naye
Bw. Ruge Mutahaba kwa upande wake alieleza kufurahishwa na fursa
mbalimbali zinazopatikana Comoro na kuahidi kuendelea kushirikiana na
Ubalozi wa Tanzania Visiwani hapa kuhakikisha kwamba FURSA EXPO Comoro
inafanikiwa na kuleta matokeo chanya kwa lengo la kuinua uchumi wa
vijana wa Kitanzania na wa KiComoro.
Post a Comment