ad

ad

ABB KUMALIZA TATIZO LA UMEME NCHINI


Mmoja wa wataalamu wa ABB (katikati) akiwaeleza jambo wanahabari.

Moja ya transfoma ikiwa kazini kwenye gereza la Robben Island alilowahi kufungwa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.

Wanahabari wakioneshwa jenereta lililounganishwa na transfoma ya ABB ili kufua umeme wa uhakika.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ABB makao makuu, Switzerland, Harmeet Bawa (kulia) akiwafafanulia jambo wanahabari waliokuwa kwenye ziara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa ABB Afrika Kusini na nchini za Kusini mwa Afrika, Leon Viljoen akiongea na wanahabari (hawapo pichani).

Wanahabari wakikagua mitambo ya umeme wa jua 'solar' inayoongezewa nguvu na transfoma za ABB ambayo hutumika kwenye gereza la kumbukumbu la Robben Island.

Harmeet Bawa (kulia) akiwafafanulia jambo wanahabari kushoto ni Leon Viljoen.

Mmoja wa Watumishi wa ABB Afrika Kusini, Tamara Chetty (kulia) akiwa kwenye msafara wa wanahabari haupo (pichani) kushoto ni mmoja wa wanahabari wa nchini Afrika Kusini.


Mradi mkubwa wa teknolojia ya kisasa ya kuongeza nguvu umeme unatarajiwa kuzinduliwa na kampuni ya kutengeneza tranfomer ya ABB ambayo imeshamaliza tatizo hilo katika nchi zaidi ya 100 ulimwenguni ikiwemo Afrika Kusini.

Akizungumza na wanahabari wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali kwenye mkutano uliofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Table Bay jijini Cape Town, Mkurugenzi Mtendaji wa ABB nchini Afrika, Leon Viljoen, alisema teknolojia ya kisasa ya kampuni hiyo imemaliza tatizo sugu na umeme nchini humo ikiwemo kisiwa chenye gereza la kihistoria alilowahi kufungwa mpigania ukombozi, Nelson Mandela la Robben Island.

Katika ziara hiyo wanahabari walitembezwa sehemu mbalimbali kuangalia mazingira ya nchi mji huo na kufika mpaka kwenye kituo cha kudhibiti umeme cha serikali katika jiji la Cape Town ambapo msemaji kituo hicho aliwaeleza wanahabari jinsi ABB walivyoisaidia serikali hiyo kupata umeme wa uhakika kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo viwandani visiwani na sehemu nyine zinazohitaji umeme wa kutosha.

Msemaji huyo alielezea nchi hiyo ilivyokuwa ikipata shida ya umeme kabla ya kuanzishwa mradi huo unaoshirikiana na serikali ya Afrika Kusini.
Baada ya kusema hayo Viljoen amesema baada ya kuondoa tatizo la umeme nchi mbalimbali hivi karibuni kampuni hiyo inatarajia kuzindua huduma hiyo nchini Tanzania na Zambia.

Viljoen amesema transfoma za kampuni yao zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo zinasapoti umeme wa gridi ya taifa, jenereta, maji, jua na nyinginezo jambo ambalo litaweza kuondoa tatizo la umeme kwenye visiwa, vijiji na sehemu ambazo hazijafikiwa na gridi ya taifa.

No comments

Powered by Blogger.